sep
07
2015

Usafi wavaliwa njuga kwenye vituo vya mabasi kaskazini mwa Mji Bujumbura

Wanamemba wa Shirika ACBN wamekutana hiyo jumapili kutathimini msimamo wa Shirika. Baada ya kusomewa hali ya kiuchumi, walionyesha malalamiko yao kuhusu kamati ya kufuatilia matumizi ya mapato ya Shirika. Walipendekeza kuchaguliwe kamati nyingine inayofaa na huenda itaheshimisha kazi itakayopewa. Haswa, kamati hiyo inashtakiwa kutotenda vema kazi yao na walisema kuwa na uhakika kwamba kamati ya leo haijui ni wapi magari yanalala, ubovu yaliyonayo pamoja na namna pesa zinavyoingia zikiwa zile za michango ama zile za mapato kulingana na kutumika kwa magari ya Shirika.

Pamoja na hayo, swala lililochambuliwa kwa undani ni lile la usafi mdogo. Washiriki wamelalamikia kuona kwenye kituo cha mabasi karibu na kanisa katolika “Saint Michel” hapana vyoo vya kujisaidia. Wamesema kwamba ni mahari panapo kusanya magari na watu wengi na wanakojolea kwenye kuta za nyumba za watu. Hiyo ni aibu. Baada ya kulichambuwa kwa undani, wamepeana miezi isiyozidi mitatu vyoo viwe vimekwisha jengwa.

Kwa ngambo hiyo ya usafi, madreva na kondakta wametakiwa kuvaa vizuri wakiwa kazini kuheshimu abiria. Pia, wamekatazwa kuvutia bangi vituoni ama kutumia pombe walizoziita pombe chafu “kanyanga”. Kuheshimisha wajibu huo, kumeteuliwa kamati ya watu sita kufanyia kazi swala hilo vituoni la usafi na walipewa mwezi mmoja kulivalia njuga.

Kwa upande mwingine, walisema kufurahia kiwango Shirika linachofikia. Pongezi zilimwendea kiongozi wa ACBN kulingana na ushuja wake. Kwa maana hiyo, kiongozi, Ernest MIBURO, ameteuliwa mhula mwingine wa miaka mitano. Kama kiongozi wa zamani Ernest ameteuliwa upya ametaja miradi mipya ya kuinua Shirika. Pamoja na hiyo ni kuimarisha umoja katika wanashirika, kuhimiza wanashirika kujikwamua kutoa michango. Na ni wakati mwafaka kuwapokea wanamemba wapya katika Shirika ACBN. ACBN (Association des Chaffeurs des Bus Nord ville) ni Shirika la wabeba abiria kaskazini mwa Mji Bijumbura wakitumia mabasi.

Langues: 
Genre journalistique: 
Thématiques: 

Partager